“Unajua mimi najua nilipotoka mpaka nilipofika hapa naweza kusema I made it, wakati mama yangu ana ujauzito wangu wa miezi sita baba yangu mzazi alifungwa jela miaka miwili hivyo mama alipambana kwa kuuza maandazi na vitumbua mpaka nazaliwa na kunilea hivyo leo kwa hapa nilipofika huwa napenda kushare historia yangu ili watu wajue,” alisema Ben Pol.
Mbali na hilo Ben Pol anasema kuwa yeye hakuzaliwa hospitali bali mama yake mzazi wakati wa kumzaa yeye alijifungua akiwa nyumbani.
